Ruka hadi kwenye maudhui makuu
MASTER SHIVO NA UJIO WA FILAMU KIMATAIFA
Star wa mchezo wa shaolin cung fuu ametoa gumzo kwa watanzania kitu ambacho hakuna aliyetarajia wala kuamini.Swala lililozua gumzo ni pamoja na kuunganisha mawasiliano kwa kuweka mahusiano bora ya kikazi katika utengenezaji wa filamu kwa kiwango cha kimataifa na wasanii mashuhuri duniani kama Jean Cloud van Damme ambaye ni supperstar kimataifa pamoja Janson Startum wasanii wa hollywood.Master Shivo anasema pia pamoja na kupewa hongera na wasanii hao wa kubwa kumemfanya apate nguvu ya kuongeza kasi kwenye tasnia ya filam Tanzania ili kuleta heshima kubwa ndani ya nchi yetu. Na ameandaa filamu ita kayokwenda kwa jina la Fire's Bligedier ambayo ni filamu ya action itakayoendelea kumtambulisha kimataifa mara baada ya kucheza filamu inayokwenda kwa jina la NO ONE.
Master Shivo aliongeza kwa kusema kuwa hana mtu wa kushindana nae ndani ya nchi badala yake ushindani wake utakuwa na wasanii wa kimataifa.bila kusita alieleza kuwa tasnia ya filam ndani ya nchi yetu inaendelea kushuka siku hadi siku kutokana na wasanii wenyewe kwa wenyewe kukosa ushirikiano
''Binafsi nimejipanga kulikabili soko la filamu la dunia bila kuogopa kwakuwa tayari nimefanya muunganiko na wasanii ambao binafsi sikutarajia lakini ndo yamekuwa nipo vizuri katika mapambano katika kuinua tasnia hii ya filam ndani ya nchi yangu ya Tanzania na kwa ushirikiano wa viongozi wangu wa nchi''.
Shukrani kwa Manani ,Niwapongeze wazazi wako kwa kukulea vizuri ,pia
JibuFutaHongera kwa bidii ya kazi ya ukuzaji wa filamu za kitanzania na kuongeza ajira kwa wanajamii na ujirani.ikiwa ni pamoja na kuwa na dira ya kushiriki katika ulimwengu.
NO ONE ni Filam nzuri ya ujasiri na vitendo ,ongezea sauti za wazungumzaji,
Mtu aliyekimbia na mfuko hatukufahamu alikuwa na nini je,pesa,dhahabu au kitu cha thamani kilichopelekea kutumia siraha hizo.
Mtazamo wako ni mzuri ,utatimiza njozi zako za kimataifa.Manani akufungulie zaidi.